Home news NYOTA WAPYA SIMBA ISHU YAO KUTUMIKA KIMATAIFA SIMBA WATOA TAMKO HILI

NYOTA WAPYA SIMBA ISHU YAO KUTUMIKA KIMATAIFA SIMBA WATOA TAMKO HILI


UONGOZI wa Simba umethibitisha kuwa 
wachezaji wake wote wa kimataifa waliosajiliwa tayari wamepokea Hati za Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa ajili ya kushiriki michuano ya kimataifa wakiwemo mastaa Pape Ousmane Sakho na Peter Banda.

Simba tayari imefanya usajili wa wachezaji watano wa kimataifa ambao ni Mmalawi, Peter Banda, Msenegal Pape Ousmane Sakho, Mmalawi, Duncan Nyoni, Msenegal Sadio Kanoute na Mcongo, Henock Inonga Baka.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu, alisema kuwa wachezaji wote wa kimataifa wa klabu hiyo ambao wamewasajili, wote wameshapata hati zao kwa ajili ya kuitumikia klabu hiyo, hivyo wanayo ruhusa ya kuwatumia katika michuano yote watakayoshiriki msimu ujao.

“Wachezaji wote wa Simba ambao tumewasajili msimu huu wameshapata hati zao kwa ajili ya kuitumikia Simba katika michuano yote, hivyo hakuna mchezaji yeyote wa Simba ambaye tumemsajili msimu huu atashindwa kutumika ndani ya Simba kwa ishu ya vibali.

“Kila kitu kipo sawa, mashabiki wa Simba wanatakiwa kuwa na amani juu ya wachezaji wa Simba, uongozi wa Simba ni makini na unafanya vitu kwa kuzingatia kila kitu ambacho kinatakiwa kikamilike kwa wakati sahihi,” alisema kiongozi huyo.


SOMA NA HII  SIKU CHACHE KUELEKEA MECHI NA ASEC MIMOSAS...WAWA AIBUKA NA HILI KWA SIMBA...