Home Azam FC AZAM FC MIKONONI MWA WAMISRI KIMATAIFA

AZAM FC MIKONONI MWA WAMISRI KIMATAIFA


 WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Azam FC watakutana na Pyramid baada ya kumaliza ile ngwe ya kwanza ambayo ilikuwa ni dhidi ya Horseed FC.


Azam FC imeshinda kwa jumla ya mabao 4-1 mbele ya Horseed FC na kuwafanya wasonge mbele raundi ya kwanza.

Sasa Azam FC itakutana na Pyramid ya Misri katika mchezo wa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo mchezo wa kwanza utachezwa Uwanja wa Azam Complex kati ya Oktoba 15-17 mwaka huu.


Mchezo wa marudiano utafanyika Misri kati ya Oktoba 22-24 mwaka huu 2021.


Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa wanatambua ushindani utakuwa mkubwa ila wanahitaji kufanya vizuri zaidi.

“Tunahitaji matokeo mazuri, kushinda mbele ya Horseed ilikuwa ni mipango mizuri ya benchi la ufundi, unaweza kuibeza timu tuliyoshinda mbele yao lakini ina wachezaji wengi wazuri,” .
SOMA NA HII  SIMBA SC KUMBE NI MAKAO MAKUU YA AZAM FC...AMRI KIEMBA AFICHUA SIRI HII