Home Habari za michezo SAKATA LA MAYELE KUTUMIWA MAJINI….BOSI WAKE AIBUKA UJUMBE HUU KWA YANGA…

SAKATA LA MAYELE KUTUMIWA MAJINI….BOSI WAKE AIBUKA UJUMBE HUU KWA YANGA…

Habari za Michezo

Meneja wa Mshambuliaji kutoka DR Congo na Klabu ya Pyramids ya Misri Fiston Kalala Mayele aliyemleta Tanzania Nestor Mutuale, ameingilia kati sakata la mchezaji huyo la kuishutumu Young Africans na kuibua taharuki katika Mitandao ya Kijamii.

Akizungumza kwa njia ya Simu kutoka DR Congo Mutuale amesema kuwa, endapo madai yanayoenea yatakuwa yametoka kwa Mayele, Mshambuliaji huyo atakuwa ameikosea heshima klabu yake hiyo ya zamani ya Young Africans.

Mutuale amesema hata kama Mayele atakuwa amekasirishwa na shabiki mmoja wa soka, au kiongozi fulani, hakuwa sahihi kuisema vibaya timu ya Young Africans ambayo ina mchango mkubwa kwenye maendeleo yake.

“Nimeona mitandao ya Tanzania inasema hayo mambo kwamba Mayele anaisema vibaya Young Africans, sijaongea naye tangu wamerudi hapa nchini kutoka Ivory Coast, lakini kama kweli hayo maneno ameyasema yeye atakuwa ameikosea heshima Young Africans,” amesema Mutuale.

“Wachezaji hawatakiwi kuwajibu mashabiki hasa mitandaoni, shabiki anaweza kusema lolote, mchezaji unatakiwa kuvumilia na kuendelea kufanya kazi yako, kule uwanjani ndio unatakiwa kuwajibu mashabiki.

“Young Africans haiwezi kufanya kitu kibaya kwa Mayele, kama kuna shabiki amemtolea lugha chafu Mayele atakuwa amekosea lakini Mayele kuisema vibaya Young Africans ni makosa makubwa amefanya.

“Unajua Young Africans imefanya makubwa kwa Mayele, ule upendo walimpa ni wa kiwango kikubwa sana, wapo watoto wakubwa, viongozi na maelfu ya mashabiki wamekuwa wakimpenda Mayele kutokana na kazi yake, unapotaka kusema kitu kibaya kuhusu mtu mmoja unatakiwa kuwaangalia hawa wengi watajisikiaje.

Aidha, Mutuale amewataka mashabiki wa Young Africans kumsamehe Mayele kwani atakuwa amejifunza kuwa amekosea kwani bado ni mtoto wao ambaye siku moja wanaweza kukutana naye tena.

“Mimi nitamtafuta Mayele nitaongea naye, nimeongea na viongozi wa Young Africans wamesikitika, lakini nimewaambia wamsamehe Mayele na mashabiki nao wamsamehe ni mtoto wao amewakosea hawawezi kusema sio ndugu yao tena, maisha yanaweza siku moja tena yakamfanya arudi tena nyumbani kwao.

Mitandao ya kijamii imelipuka kwa watu kufanyiana utani kwamba wanayanga wanamfanyia hujuma Mayele asifunge mabao katika klabu yake ya Pyramids na timu yake ya taifa ya DR Congo.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMAPILI