Home Habari za michezo BAADA YA KUMRUDISHA KISINDA NYUMBANI….YANGA HAWAJALAZA DAMU AISEE…WAMPA KAZI HII KUBWA YA...

BAADA YA KUMRUDISHA KISINDA NYUMBANI….YANGA HAWAJALAZA DAMU AISEE…WAMPA KAZI HII KUBWA YA KUFANYA…

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Yanga SC, Simon Patrick amesema kuwa Klabu hiyo imekamilisha usajili wa mashindano yote ikiwemo Ligi Kuu Bara, Ligi ya Mabingwa pamoja na usajili wa Yanga Princes.

Kupitia mtandao wake wa Kijamii wa Instagram Simon ndika kuwa;

Dirisha la usajili limefungwa rasmi, sasa tuko tayari kwa mapambano ya msimu huu wa 2022/2023, ni vyema kwa Mwanayanga kuyafahamu yafuatayo;

1.Klabu ya Yanga imekamilisha usajili wake wote kwa mashindano ya ndani na ligi ya mabingwa Afrika.

2.Kwa mujibu wa Club licensing ya CAF mwaka huu, ili timu iruhusiwe kucheza Mashindano ya Klabu bingwa Afrika ni lazima iwe na timu ya Wanawake na program ya timu za vijana.

3.Klabu ya Yanga itaanza kucheza mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika tarehe 10/09/2022 dhidi ya Zalan FC Rumbek (South Sudan) kwenye dimba la Chamazi kama mchezo wa ugenini.

4.Usajili wa Carbon 14 ndio unatufungia rasmi usajili wa dirisha hili kubwa, surprise hii ni zawadi kwa Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa Yanga kwa kuendelea kuipa support na thaman klabu yetu.

5.Malengo yetu msimu huu ni kutetea makombe yote ambayo tumeshinda msimu uliopita na kufika angalau makundi kwenye klabu bingwa Afrika.

SOMA NA HII  WAKATI WATU WAKIITAJA GSM TU KWENYE MAFANIKO YA YANGA...MANARA AIBUKA NA 'KUWAZODOA' KWA HILI...