Home Habari za michezo BAADA YA KUMALIZANA NA WAARABU…MSUVA AZIITA SIMBA NA YANGA…AZAM HUENDA WAKAFANYA KWELI…

BAADA YA KUMALIZANA NA WAARABU…MSUVA AZIITA SIMBA NA YANGA…AZAM HUENDA WAKAFANYA KWELI…

Habari za Michezo

Mshambuliaji wa timu ya taifa, Taifa Stars, Simon Msuva amejiweka sokoni akieleza kuwa anakaribisha ofa baada ya kumaliza mkataba wake katika timu ya Al Qadsiah inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Saudi Arabia.

Msuva ameyasema hayo baada ya kuisaidia Stars kuibuka na ushindi wa 1-0, dhidi ya Niger, katika mchezo wa kuwania kufuzu kushiriki Afcon 2023 uliopigwa Jumapili (Juni 18).

Mchezaji huyo amesema kwa sasa yuko huru baada ya kumaliza mkataba wake wa mwaka mmoja na timu hiyo aliyojiunga nayo mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea Wydad Casablanca ya Morocco.

Mchezaji huyo aliyewahi kukipiga Young Africans, amefunguka kuwa ingawa yuko tayari kusikiliza ofa mbalimbali kwa maana hata ya timu kongwe na maarufu nchini za Simba SC, Young Africans na Azam FC lakini amebainisha kuwa bado ana ndoto ya kucheza nje ya nchi.

“Kuhusiana na usajili niseme kule nimeshamaliza mkataba, nilisaini mwaka mmoja na sasa umeshaisha, kwa hiyo nipo huru.

Nakaribisha ofa za ndani na za nje maana ofa hazikataliwi japo nina ndoto za kuendelea kucheza nje,” amesema Msuva.

Msuva aliyeibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2016-17, alijiunga na Qadsiah baada ya mgogoro wake wa kimaslahi na Wydad aliyoshinda nayo makombe mawili ya Ligi Kuu ya Morocco maarufu Botola Pro.

Awali wakati wa mgogoro wake na Wydad, Msuva alitajwa kuwaniwa na baadhi ya timu nchini kutokana na uzoefu mkubwa alionao na soka la Afrika kwa ujumla kabla ya kuamua kutimkia Saudia.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA KUFUKUZWA YANGA...NABI AVUNJA UKIMYA..ADAI YUKO TAYARI HATA SASA 'KUSEPA...'

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here