Home epl MAANDAMANO YA MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED YAUMIZA POLISI

MAANDAMANO YA MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED YAUMIZA POLISI


NGUVU ya mashabiki wa Klabu ya Manchester United ambao walikuwa wanapinga utawala wa familia ya Glazer wakitaka ujiondoe madarakani zimesababisha mchezo wa Ligi Kuu England kati ya timu hiyo dhidi ya Liverpool kughairishwa.

Miongoni mwa sababu ambazo zimewafanya mashabiki hao kuipinga familia ya Glazer ni pamoja mpango wao wa kuingia katika European Super League Cup kisha kujitoa na kusababisha kupigwa faini jambo ambalo haliwafurahishi mashabiki hao kwa kuwa wanaona ni hasara.

Pia wanadai kwamba familia hiyo ya Marekani haijawa na mafanikio mazuri hasa kwenye upande wa kutwaa mataji jambo ambalo wanaamini utawala huo hauna manufaa kwao bali ni kwa maslahi ya viongozi hao hasa katika masuala ya uchumi.

Licha ya Polisi kutumia nguvu kuwatuliza mashabiki hao bado haikuweza kuwa rahisi na imeripotiwa kwamba Polisi wawili walijeruhiwa katika purukushani hizo na mchezo huo utapangiwa tarehe nyingine baada ya kuahirishwa.

SOMA NA HII  CHELESEA YAWEKEWA NGUMU KUMPATA HAALAND