Home Habari za michezo MANGUNGU:- TUTAWAFUNGA YANGA MPAKA SIKU NAONDOKA SIMBA….

MANGUNGU:- TUTAWAFUNGA YANGA MPAKA SIKU NAONDOKA SIMBA….

Habari za Simba

Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu amesema ahadi aliyotoa kwenye uchaguzi mkuu wa klabu hiyo ya kuifunga Yanga itaendelea kwa miaka minne mpaka atakapoondoka madarakani.

Akizungumza nasi, kiongozi huyo amesema watu wengi ikiwemo mashabiki wa Yanga, walimponda na kumbeza, lakini athari yake imeonekana  baada ya kipigo cha mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

“Wakati natoa ahadi ile sikuwa na bahatisha, nilikuwa na uhakika na timu yangu na Yanga wanatakiwa kujua kwamba pale siyo mwisho tutaendelea kuwafunga hadi niondoke madarakani, ndio ahadi inaisha,” amesema Mangungu.

Mangungu anatarajiwa kuiongoza Simba, hadi Januari 2026 kipindi ambacho uongozi wake utafika kikomo baada ya kufanyika kwa uchaguzi mpya.

SOMA NA HII  INFANTINO:- KAMA POMBE NI MUHIMU KULIKO KOMBE LA DUNIA...NAWAACHIA FIFA YENU...