Home Habari za michezo KIPIGO CHA YANGA CHAZUA VITA MPYA MJINI…JEMEDARI AMPIGA ‘DONGO’ LA MWAKA MANARA…

KIPIGO CHA YANGA CHAZUA VITA MPYA MJINI…JEMEDARI AMPIGA ‘DONGO’ LA MWAKA MANARA…

Habari za Yanga

Baada ya Yanga kupokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Simba katika mchezo wa Dabi ya Kariakoo.

Jemedari Said amemtupia kijembe aliekuwa msemaji wa Yanga Haji Manara ambae aliwahi kutamba huko nyuma kwamba ataweza kufungwa na Yanga.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Jemedari ameweka Video Clip ya Manara na kuandika;

“Kuna wakati tunaamini wajinga kwenye mambo ya msingi mpaka wanajiona “miungu watu”, ishatokea sasa inakuaje?

Mpira unataka heshima, derby inataka heshima. Mzee Kaduguda aliwahi kusema huwezi kuwafunga Yanga kama hauwaheshimu, manake Yanga wanaweza wakaokotana wazee kama yeye 11 wakaingia kiwanjani wakaifunga Simba.

Huyo ni mwandishi wa habari mkongwe nchini, Katibu Mkuu wa zamani wa FAT (sasa TFF), Mwenyekiti wa zamani wa Simba SC na mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, Mwenyekiti wa zamani wa Ghymkhana club Dar es Salaam na msomi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam anaonyeaha kuheshimu mpira na miiko yake, halafu mjinga mmoja anasema yeye hawezi kufungwa mpaka anakufa na watu wanashangilia na kuamini, ndo nchi yetu sasa tufanyeje? Tunapawa kuachana na wadananda hawa hawajui boli wanaganga matumbo yao tu”.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUDORORA MSIMU HUU...SIMBA WAZIDI KUTAKATA VIWANGO VYA CAF....YANGA HAIONEKANI ETI....