Home Yanga SC YANGA KUMSHUSHA MSHAMBULIAJI WAO MWILI JUMBA MUDA WOWOTE

YANGA KUMSHUSHA MSHAMBULIAJI WAO MWILI JUMBA MUDA WOWOTE


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa nyota wao Michael Sarpong anatarajiwa kurejea muda wowote kuanza sasa baada ya kumaliza muda wake wa mapumziko.

Sarpong, wengi wanapenda kuwmita mwili jumba, ametupia mabao manne ndani ya Ligi Kuu Bara alitarajiwa kurejea jana kujiunga na kikosi kambini ila kuna mambo yalikwamisha mpango huo.

Meneja wa Klabu ya Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa nyota huyo atarejea muda wowote kuanza sasa.

“Tayari kikosi kimeanza mazoezi baada ya kuwasili kambini jana, Januari 25 hivyo bado kuna wachezaji ambao wanawasili kambini.

“Kuhusu Sarpong bado ni mchezaji wetu na anatarajiwa kurejea muda wowote kuanza sasa kwa kuwa alikuwa kwenye mapumziko, nchini Ghana,” amesema. 

SOMA NA HII  'SURE BOY' APEWA ONYO KALI MECHI YA KESHO DHIDI YA SIMBA....BABA YAKE KAIBUKA NA HILI...