Ofisa Habari wa Yanga, Alikamwe amedai kuwa wapinzani wao Al Merrikh wameanza kuwasifu kuwa Wananchi wanaogopeka Afrika wao wamesoma Cuba wanajua huo ni Mtego
“Tumesikia kauli za Kocha wa Al-Merrikh anasema kuwa Young Africans inaogopeka Afrika. Sisi tumesoma Cuba, tunamwelewa, hawezi kutuchota, tutauchukulia mchezo wetu wa pili kwa umakini mkubwa.
Amesema pia; “Wanakuja kufunguka hapa, kwetu sisi ni taarifa njema kwa sababu mnara haukusoma Rwanda, hivyo tukipishana nao itakuwa fursa ya kusimamisha mnara.”