Home Simba SC SIMBA YAMPA KAKOLANYA POLE, SISI SOTE NI FAMILIA,POLE KAKOLANYA

SIMBA YAMPA KAKOLANYA POLE, SISI SOTE NI FAMILIA,POLE KAKOLANYA


DIDER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa msiba alioupata kipa wao namba mbili ni wa familia nzima ya Simba kwa kuwa wanaishi kwa upendo amani na ushirikiano.

Jana, Agosti 19, taarifa iliyotolewa na Simba ilieleza kuwa nyota wao Beno Kakolanya amepata msiba wa mamayake.

Kutokana na msiba huo wa mama yake anayeitwa Eva Mwankusye Simba SC imempa Kakolanya ruhusa ya kurejea nchini kwa ajili ya kushiriki katika msiba huo.

Kwa sasa kikosi hicho kimeweka kambi nchini Morocco ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya wa 2021/22 unaotarajiwa kuanza Septemba 29 na Septemba 25 unatarajiwa kuchezwa mchezo wa Ngao ya Jamii.

Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa ni jambo linalowahusu wote kwa sababu wanaishi wakiwa ni familia.

“Tatizo ambalo amelipata Beno Kakolanya ni letu sote hivyo tunamuombea na tunampa pole kwa sababu sisi sote ni familia,” amesema.

SOMA NA HII  ZA CHINI YA KAPETI....MAJERAHA YA GOTI LA LWANGA SI MCHEZO...DAKTARI SIMBA AKWEPA MTEGO..MKUDE ATAJWA..