Home Habari za michezo MCHAMBUZI :- MZAMIRU HASTAHILI TUZO MBELE YA AUCHO…APEWE TUZO YAKE BINAFSI..

MCHAMBUZI :- MZAMIRU HASTAHILI TUZO MBELE YA AUCHO…APEWE TUZO YAKE BINAFSI..

Habari za Simba sc

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini Justine Kessy, amedai kuwa kiungo wa Simba, Mzamiru Yassin hakupaswa kuwa kwenye orodha ya wachezaji wanaowania tuzo ya kiungo bora wa Mwaka.

Justine Kessy amesema hayo baada ya kuibuka mjadala kuhusu kuachwa kwa kiungo wa Yanga, Khalid Aucho huku akibainisha kuwa kwa maoni yake, Aucho amekuwa bora katika msimu huu ikilinganishwa na Mzamiru.

“Ukitazama kiungo cha Yanga, kwa asilimia kubwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi huwezi kumwacha Khalid Aucho. Amekuwa engine kubwa sana kwenye kiungo cha timu hiyo msimu huu”

“Kwakuwa Mzamiru atakuwa amezidiwa na namba zangu mimi ninazozitazama kwa kiungo iwe mkabaji au mshambuliaji, hakustahili kwenye kuwania tuzo ya kiungo bora. Nadhani alistahili tuzo ya mchezaji aliyeboresha kiwango ‘most improved player’ kama ingekuwepo,” amesema Justine Kessy.

SOMA NA HII  BAADA YA YANGA KUILALAMIKIA SIMBA KWA KUISUSA MECHI YA LEO...AHMED ALLY KAWAJIBU HAYA KIBABE...