Home Habari za michezo WAKATI MASHABIKI SIMBA WAKINUNA…KIBADENI AOMBA JEZI YA YANGA AKAFANYE KAZI YAKE MAPEMA…

WAKATI MASHABIKI SIMBA WAKINUNA…KIBADENI AOMBA JEZI YA YANGA AKAFANYE KAZI YAKE MAPEMA…

Habari za Michezo

Kocha na mchezaji wa zamani wa Simba, Abdallah Kibadeni amesema yupo tayari kuvaa jezi ya kijani na njano, ili kuipa sapoti Yanga, iweze kubeba ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger.

Akizungumza nasi, Mkongwe huyo amesema ana imani kubwa na Yanga kuanzia uongozi, benchi la ufundi na hata wachezaji hivyo anachowataka watumie faida ya kucheza nyumbani ili kushinda idadi kubwa ya mabao na kujiondoa kwenye presha watakapokwenda ugenini katika mechi ya marudiano.

β€œMwaka 1993 nilikuwepo kwenye kikosi cha Simba kilichocheza Fainali na Stella Abidjan kifupi tulifanya makosa ya kushindwa kutumia vizuri uwanja wa nyumbani baada ya kuonesha kiwango bora kule Ivory Coast, sasa sipendi wenzetu Yanga warudie makossa hayo,” amesema Kibadeni.

Yanga itacheza na USM Alger leoΒ  Jumapili ikiwa ni mchezo wa mkondo wa kwanza wa Fainali ya Kombe la Shirikisho, huku fainali ya pili ikipangwa kuchezwa Juni 3 huko nchini Algeria.

SOMA NA HII  KOCHA TAIFA STARS ALIVYOAMUA KUBADILI UPEPO KAMA UTANI