Home Habari za michezo GAMONDI AGOMA KUSHUKA KUTOKA KILELENI ATOA KAULI HII

GAMONDI AGOMA KUSHUKA KUTOKA KILELENI ATOA KAULI HII

Habari za Yanga SC

Kocha Mkuu wa Young Africans, Miguel Angel Gamondi amesema kuwa hataki kuondoka katika kilele cha msimamno wa Ligi Kuu Bara huku akiuchukulia kila mchezo uliokuwepo mbele yake kama fainali.

Hiyo huenda ikawa salamu kwa Simba SC ambao wamepanga kuwapoka Young Africans taji la Ligi Kuu Tanzania Bara walilolichukua misimu miwili mfululizo wakiwa na Kocha Mkuu Mtunisia, Nasreddine Nabi.

Young Africans inaongoza katika msimamo wa ligi ikiwa na alama 18, ikifuatiwa na Simba SC yenye alama 15 na leo itashuka dimbani kucheza dhidi ya Ihefu FC.

Gamondi amesema kuwa amekaa na wachezaji wake na kumsisitiza kila mchezaji atakayepata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza anatimiza vema majukumu yake ya uwanjani.

Gamondi amesema ubingwa wa msimu huu hautakuwa mwepesi tofauti na misimu iliyopita kutokana na kila timu kuipania Young Africans, kwa kucheza kwa bidii kwa lengo la kutaka kuwafunga.

Ameongeza kuwa ameliona hilo mapema, na kuwataka wachezaji wake kila mchezo kucheza kama fainali, kwa lengo la kupata pointi tatu ili malengo yao yatimie ya kutetea taji hilo.

“Hatutaidharau timu yoyote tutakayokutana nayo katika ligi, ni kutokana na kila timu inabadilika inapokutana dhidi ya Young Africans, inatumia nguvu nyingi kwa kucheza kwa kutupania, kwa lengo la kutufunga.

“Kama kocha nimechukua tahadhari mapema ya hilo, kwa kuwataka wachezaji wangu wanacheza kila mchezo wa ligi kama fainali kwa lengo la kupata pointi tatu zitakazotubakisha kileleni katika msimamo.

“Ninataka kuona tukipata ushindi katika kila mchezo utakaokuwepo mbele yetu, nimewasisitiza juu ya hilo wachezaji wangu wote kwa kuanzia mchezo wetu wa jana dhidi ya Singida Big Stars,” amesema Gamondi.

SOMA NA HII  MOLINGA AKUNJA JAMVI LAKE YANGA, KUIBUKIA MOROCCO