Home news ‘FEI TOTO’ ASHINDWA KUJIZUIA YANGA…AAMUA KUFUNGA MAPYA KUHUSU UBINGWA KUTUA JANGWANI…

‘FEI TOTO’ ASHINDWA KUJIZUIA YANGA…AAMUA KUFUNGA MAPYA KUHUSU UBINGWA KUTUA JANGWANI…


KIUNGO Mshambuliaji wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ameweka wazi kuwa wao kama wachezaji wanaendelea kujipanga kuhakikisha wanapata alama tatu kwenye michezo yao inayofuata kwani msimu huu wana jambo lao hivyo mashabiki wasiwe na wasiwasi.

Yanga hadi sasa inaongoza Ligi Kuu Bara kwa pointi 16 katika michezo yote sita iliyocheza hadi sasa huku ikifuatiwa na Simba wenye pointi 14.

Akizungumza na Championi Jumatano, Feisal alisema kuwa kama safari ndio kwanza imeanza ya kusaka ubingwa, hivyo wamejipanga vizuri kuhakikisha wanapata alama tatu kwenye mechi zao zinazofuata.

“Tunamshukuru Mungu hadi hapa tulipofikia tunaongoza ligi lakini hiyo pekee haitoshi kutufanya turidhike, hivyo tunaendelea kupambania malengo ya timu kwa sababu sisi wachezaji ndio tuna dhamana kubwa ya kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri kwa kupambana uwanjani.

“Kwa hiyo kitu pekee ninachoweza kuwaambia mashabiki wetu wasiwe na wasiwasi kwani tumejipanga vizuri sana msimu huu tuna jambo letu kubwa ambalo kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu litatimia,” alisema mchezaji huyo.

SOMA NA HII  KIGOGO YANGA- TUNAPASWA KUWAIGA SIMBA SC KIMATAIFA