Home Habari za michezo IMEFICHUKA…YANGA WATUMIA MAMILIONI HAYA KUKODI GARI LAO LA UBINGWA UGANDA…DEREVA AFUNGUKA A-Z…

IMEFICHUKA…YANGA WATUMIA MAMILIONI HAYA KUKODI GARI LAO LA UBINGWA UGANDA…DEREVA AFUNGUKA A-Z…


Yanga wametisha sana! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema. Moja kati ya vivutio katika sherehe za Ubingwa wa Klabu ya Yanga ni pamoja na basi la wazi ambalo wamelikodi kutokea Uganda kuja nchini Tanzania katika parade ya Ubingwa.

Sasa kutokana na tukio hilo la aina yake, watu wengi wamekua wakihoji na kutamani kujua gharama za kuleta basi hilo nchini kwa siku ni kiasi gani.

Dereva wa basi hilo ameweka wazi kuwa, kwa makadirio, kukodi basi hilo ni kiasi cha dola za Marekani 1,000 (Tsh milioni 2.3) kwa siku.

Dereva huyo amesema basi hilo kwa Uganda limekuwa likitumika kwa ajili ya kufanya tour za mjini na za shule, sherehe mbali mbali zikiwemo harusi, za kuzaliwa na hata mikutano vyote vinafanyika ndani ya basi.

Dereva huyo amefafanua kuwa aliwahi kuja Tanzania kama abiria, lakini kuja na gari hiyo kwa shughuli hizo za mpira kwake ni mara ya kwanza na kwamba jambo hilo ni zuri sana na hajawahi kuona kwao Uganda.

“Ni jambo zuri sana, aina ya mashabiki na sapoti wanayotoa kwa timu kama hivi, sijawahi kuona,” alisema dereva huyo.

SOMA NA HII  WAKILI WA YANGA, AWAPIGA DONGO HILI SIMBA SC, MANGUNGU AHUSISHWA