Home Uncategorized MFUMO MPYA WA SIMBA SASA KIBOKO,PUNGUZO KWA TIKETI MPAKA ASILIMIA KUMI

MFUMO MPYA WA SIMBA SASA KIBOKO,PUNGUZO KWA TIKETI MPAKA ASILIMIA KUMI

erified

SIMBA leo wametangaza kuingia mkataba mwingine na benki ya Equity ambao una malengo ya kusimamamia mradi wa kadi mpya za za wanachama na mashabiki zitakazoitwa Simba Card.

Kupitia ukurasa wa Instagram wameandika namna hii:-“Tumeingia mkataba na benki ya Equity ambao utawezesha benki hiyo kusimamia mradi wa kadi mpya za wanachama na mashabiki ambazo zitaitwa Simba Card.

“Kadi hizo zitatumiwa na wanachama na mashabiki kuweka akiba ya pesa na kutoa pindi wanapotaka kutumia, lakini pia kulipa ada ya kila mwaka, kununua tiketi za kuingia mpirani, na kupata punguzo la mpaka 10% kwenye maduka makubwa ambayo tutashirikiana nayo.

“Faida kubwa kwa klabu katika kadi hizo ni makato yanayopatikana wakati wa kufungua akaunti, kukusanya ada kisasa na mara moja kwa mwaka, na kupata takwimu sahihi za mashabiki iwapo kila shabiki atafungua akaunti.

“Kadi hizo zitaanza kutolewa Septemba mosi mwaka huu kwa kuwabadilishia kadi wanachama wa sasa na baadae litaendelea kwa wanachama wapya na mashabiki,”,

SOMA NA HII  SIMBA: HATUPO LEVO MOJA