Home news SIMBA WAZIDI KUNEEMEKA…WAPATA UDHAMINI WA MABASI MAPYA ..WAPEWA MILIONI 800

SIMBA WAZIDI KUNEEMEKA…WAPATA UDHAMINI WA MABASI MAPYA ..WAPEWA MILIONI 800


Klabu ya Simba imepata udhamini mmono kutoka katika kampuni ya kuuza na kukodisha magari ya Africarriers Limited ambao thamani yake ni Sh800 milioni.

Katika udhamini huo Simba watapata mabasi matatu kwa ajili ya timu zao tatu za Simba ya vijana, Queens na ile ya wakubwa.

Mwanasheria wa Africarriers Limited, Ngas Ngaja anasema tumewahiteni hapa kwa sababu moja ya tukio kubwa sana ambalo linafunua ukurasa mpya kwa klabu ya Simba na kampuni yetu ya Africarriers Limited, na tukio hilo linausisha udhamini mkubwa.

Ngaja anasema mkataba huo wa Simba na Africarriers utakuwa na muda wa miaka minne na thamani yake itakuwa Sh800 miloni na kuwapa mabasi aina tofauti.

Anasema mabasi ambayo watawapa Simba yatakuwa matatu moja ni Golden Dragon kwa timu kubwa ambalo litakuwa na uwezo wa kubeba watu waliokaa kwenye viti 60.

“Sambamba na hilo tumetoa mabasi mengine mawili kwa timu ya Simba ya vijana pamoja na Simba Queens ambao tulikuwa tunawazamini tangu msimu uliopita,” anasema Ngaja na kuongeza;

“Kampuni yetu inahusisha na uzaji wa magari nchini Tanzania pamoja na ukodishaji tumeamua kuwapa udhamini Simba kwani tumeona kwa sasa ni timu kubwa Afrika kati ya 13, ambazo zinatajwa.

“Tumeamua tushiriki mafanikio ya klabu ya Simba na tumeona tuwaendeshe na ili kufikia mafanikio yao kuwa mabingwa wa Afrika tutakuwa tunawaendesha,” anasema Ngaja.

Ofisa mtendaji mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez anasema mkataba huu unathamani ya Sh800 kwa kupewa mabasi matatu kwa timu zetu tatu na watakuwa wanawasaidia katika mambo mengine ya msingi.

Barbara anasema wameonyesha ukubwa wa taasisi yao kwa kutaka kushirikiana na Simba leo hii kampuni kubwa kama hii imeona mchongo mkubwa wa soka na wameamua kuwekeza kwetu.

“Wameona wanaweza kutangaza bidhaa zao kupitia Simba na walifanya majaribio ya hilo kupitia kwa mlezi wetu wa Simba Queens, Fetima Dewji ambaye kwa kipindi cha miezi minne tumeona thamani kubwa,” anasema Barbara na kuongeza;

SOMA NA HII  WAKATI SIMBA WAKIMGWAYA....IHEFU NA GEITA ZAMMEZEA MATE KIBU DENIS...

“Fetema akaona kwa nini asijiongeze zaidi kwa ajili ya timu zetu nyingine kufanyiwa uwekezaji, na amefanya kazi kubwa kwani gari moja si chini ya Sh460 milioni na Simba tumepata bure kazi yetu ni kumuweka dereva na mafuta tu,” anasema Barbara.