Home news OMOG RASMI MALI YA MTIBWA SUGAR

OMOG RASMI MALI YA MTIBWA SUGAR


SASA ni rasmi, Joseph Omog raia wa Cameroon ni Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar ya Morogoro. 

Kocha huyo ametambulishwa leo Septemba 24 kwa mashabiki na wanachama wa Mtibwa Sugar.

Tayari leo ameanza kazi na vijana wake hao ambao kambi yao ipo Morogoro, mji kasoro bahari.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa wanaamini kwa uzoefu alionao pamoja na uwezo ataifanya timu hiyo kuwa na ushindani mkubwa.

“Tunahitaji kufanya vizuri tofauti na msimu uliopita, uwepo wa Omog utatufanya tuwe na mwendo mzuri na matokeo chanya,”.

Kocha huyo amewahi kuinoa Simba pia na Azam FC hivyo ana uzoefu na Ligi Kuu Bara. 

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO SIMBA SC WALIVYOFAULI NA KUFELI MECHI YA JANA DHIDI YA WYDAD....