Home news ZAHERA: – HUYU MAYELE LABDA AZEMBEE TU MWENYEWE….AFUNGUKA JINSI ANAVYOCHEZESHWA..

ZAHERA: – HUYU MAYELE LABDA AZEMBEE TU MWENYEWE….AFUNGUKA JINSI ANAVYOCHEZESHWA..


MKURUGENZI wa Soka la Vijana wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema straika wa timu hiyo, Fiston Mayele, ana kila sababu ya kuwa mfungaji bora msimu huu, labda tu azembee mwenyewe.

Zahera alisema suala la kuwa mfungaji bora kwake lipo kwa asilimia kubwa, kwa sababu amekuwa na uwezo wa kufunga kwenye kila mchezo uliopo mbele yake na kama akishindwa basi itakuwa ni uzembe wake mwenyewe.

Zahera amesema kuwa Yanga ina wapishi wengi sana kwa sasa ambao wanaweza kumpikia mabao ya kutosha Mayele na yeye akawa anafunga kirahisi, kwa hiyo ni yeye tu kuweka juhudi kwenye kila mchezo.

“Yanga ina wapishi wengi wa mabao na Mayele naona kabisa ana kila sababu ya kuchukua tuzo hiyo na hata mwenyewe niliwahi kumueleza hivyo.

“Mayele amekuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza anayecheza zaidi ya dakika 80, kila mechi tena kwenye timu iliyoimarika kuanzia kipa hadi mbele, kazi ni kwake mwenyewe ila hakuna sababu ya kumzuia na kushindwa kufanya hivyo,” alisema Zahera.

Mayele alikuwa na mabao tisa kabla ya mchezo wa jana dhidi ya Geita Gold FC, akiwa nyuma kwa bao moja dhidi ya Reliant Lusajo wa Namungo.

SOMA NA HII  MASTAA YANGA WALIOCHEZA MECHI NA IHEFU NA KUFUNGWA KUWEKWA KIKAANGONI...