Home Habari za michezo SIRI IMEFUJA SABABU ZA SIMBA KUMTEMA KIPA WAO MBAZILI…. TATIZO LIMEANZIA HAPA

SIRI IMEFUJA SABABU ZA SIMBA KUMTEMA KIPA WAO MBAZILI…. TATIZO LIMEANZIA HAPA

kipa wa simba

SIMBA imefanya maamuzi magumu ya kumpiga chini kipa Mbrazili Jefferson Luis aliyesajiliwa hivi karibuni kwa madai ya kuwa majeruhi. Japo klabu haijatoa taarifa lakini inaelezwa Jefferson amepata majeraha makubwa, hivyo amesitishiwa mkataba kwani atakuwa nje kwa muda mrefu.

Chanzo chetu cha kuaminika kinasema kwamba Jefferson alisajiliwa huku akiwa na tatizo la misuli nyuma ya paja lililogundulika juzi mazoezini, huku jina lake likiwa tayari katika usajili wa CAF. “Ni kweli amegundulika na tatizo hilo, anaweza kukaa nje kwa muda mrefu ila siwezi kusema moja kwa moja kama mkataba utavunjwa au lah! Maana maamuzi hayajafikiwa,” kilisema chanzo hicho cha kuaminika.

SOMA NA HII  AL AHLY WATUA NCHINI KUIKABILI YANGA, WAPOKELEWA NA HAPPY NATION