Home Habari za michezo BAADA YA KUPIGWA NA YANGA JUZI…TP MAZEMBE WACHUKUA MAAMUZI HAYA MAGUMU…NABI ATAJWA...

BAADA YA KUPIGWA NA YANGA JUZI…TP MAZEMBE WACHUKUA MAAMUZI HAYA MAGUMU…NABI ATAJWA HUKO…

Habari za Yanga

TP Mazembe ya DR Congo imefanya mabadiliko makubwa kwenye benchi lake la ufundi kwa kumchukua kocha wao wa zamani, Lamine Ndiaye (66) na kuachana na Pamphile Mihayo aliyepigwa na Yanga nyumbani na ugenini katika mechi za hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.

Matokeo mabaya katika hatua ya makundi ambayo TP Mazembe ilishika mkia baada ya kukusanya pointi tatu tu katika mechi sita ikiwenmo kupoteza mbili dhidi ya Yanga yameonekana kutoufurahisha uongozi wa timu hiyo chini ya tajiri Moise Katumbe na kuamua kumfuta kazi Mihayo na kumrudisha N’Diaye ambaye ana uzoefu mkubwa na soka la Afrika.

Hatua ya kumchukua N’diaye imetokana na Katumbi kushindwa kukubaliana na masharti ya kocha wa Yanga Nasreddine Nabi aliyemtaka tajiri huyo kusubiri kwa muda akigoma kuishia njiani katika msimu wa mafanikio akiiwezesha Yanga kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Katika mabadiliko hayo, N’Diaye aliyewahi kuinoa Mazembe kuanzia 2010 hadi 2013 atafanya kazi pamoja na na mafundi wengine wawili ambao Alexandre Jurain, ambaye ana uzoefu mkubwa katika mafunzo na kukuza vijana akiongozana na msaidizi wake Mathieu Mansutiea, atashughulikia maandalizi ya kimwili. Taarifa ya TP Mazembe imeeleza kuwa urejeo wa N’Diaye unalenga kuirudisha timu hiyo katika makali yake ya zamani ambayo kwa sasa yanaonekana kupotea.

“Fundi huyu ana uongozi imara na maarifa ya kimbinu ya soka na dhamira yake itakuwa kujenga upya, yaani kutekeleza mradi wa klabu kuwa na ushindani katika kiwango cha juu cha soka la bara huku ikijumuisha vipaji vya vijana hatua kwa hatua.”

“Ujuzi wake wa kiwango cha juu cha mpira wa miguu, utulivu, hisia za mazungumzo ni muhimu sana kujenga upya kikundi chenye talanta na haiba dhabiti,” ilifafanua taarifa hiyo ya Mazembe.

Muda wowote kuanzia sasa, TP Mazembe itamtambulisha rasmi Kocha huyo na mchambuzi wa Mwanaspoti mjini Lubumbashi, DR Congo, Iragi Elisha amejiridhishwa kwamba mambo mengi yameshakamilika na ni suala la muda tu kwa N’Diaye kutangazwa.

Chini ya N’Diaye, Mazembe iliwahi kushika nafasi ya pili katika mashindano ya Klabu Bingwa ya Dunia, ilitwaa taji moja la Ligi ya Mabingwa Afrika lakini pia mataji mawili ya Caf Super Cup.

N’Diaye aliipa TP Mazembe mataji matatu ya Ligi Kuu ya DR Congo na anatajwa kama miongoni mwa makocha bora wa Kiafrika kutokana na mafanikio makubwa aliyoyapata katika taaluma hiyo.

Mbali na TP Mazembe, N’Diaye amewahi kuwa kocha wa Coton Sport ya Cameroon kuanzia 2003 hadi 2006 na baadaye kuwa kocha wa timu ya taifa ya Senegal mnamo Januari 2008, kufuatia kujiuzulu kwa Henryk Kasperczak ambaye alifutwa kazi kama meneja Oktoba 2008.

Kocha huyo Msenegal aliteuliwa kuwa meneja wa timu ya Morocco ya Maghreb Fez mnamo Desemba 2008 ambayo aliitumikia hadi 2010 alipotimkia TP Mazembe.

Mnamo Desemba 2014 alikua mkurugenzi wa ufundi wa AC LĂ©opards. Kufikia Julai 2018 alikuwa meneja wa klabu ya Al-Hilal ya Sudan na Novemba 2019 alikua meneja wa klabu ya Guinea ya Horoya AC.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KESHO....MAYELE AFUNGUKA ATAKACHOWAFANYA SIMBA..."LAZIMA TIMU MOJA IPITE"...