Home Simba SC SIMBA YAWASHUSHIA AL AHLY BEI YA KUMPATA LUIS..SASA WANATAKA 650K TU

SIMBA YAWASHUSHIA AL AHLY BEI YA KUMPATA LUIS..SASA WANATAKA 650K TU


SIMBA imethibitisha ofa kadhaa mezani kwao zikimtaka staa wao, Luis Jose Miquissone lakini zikifikia dau wanalotaka wao watafanya biashara. Licha ya kutotaja majina ya klabu hizo wala ofa ya Simba, lakini Mwanaspoti linajua kwamba Bodi ya Klabu hiyo imeafikiana auzwe kwa dola 650,000 ambazo ni zaidi Sh2.1Bilioni.

Kama biashara hiyo ya Luis ikikubali kabla ya kuanza kwa msimu ujao huenda akaingia kwenye rekodi za mchezaji wa Simba aliyeuzwa ghali zaidi nje katika miaka ya hivikaribuni.

Soka la Bongo linajua kwamba miongoni mwa klabu ambazo zimeulizia uwezekano wa kumsajili Miquissone ni CR Belouizdad ya Algeria,Al Ahly ya Misri na Mamelodi Sundowns ya Sauzi.

Taarifa kutoka kwa chanzo ndani ya klabu hiyo zimefichua kuwa Simba imeamua kulegeza masharti na kuwa tayari kupokea kitita hicho tofauti na kile walichopanga awali kutokana na sababu mbili kubwa.

Sababu ya kwanza ni muda mfupi uliobakia wa mkataba wa mshambuliaji huyo lakini jambo la pili ni kutotaka kuharibu mahusiano yake na Miquissone ambaye mwenyewe ameonekana kutamani malisho mazuri zaidi ambayo ameahidiwa na timu kadhaa nje ya Tanzania.

Makamu mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ alisema kuwa wanazo ofa nyingi mezani zinazomhusu Miquissone lakini watakuwa tayari kukubali ile ambayo wataona inakidhi mahitaji yao.

“Kuna ofa kutoka timu nyingi tu za kumhitaji Miquissone lakini sisi kwa upande wetu tutakayoipa kipaumbele ni ofa ambayo itafikia dau ambalo tumeliweka na sio vinginevyo. Msimamo wetu ni huo,” alisema Try Again huku viongozi wengine wakifanya siri suala hilo mpaka watakapofikia muafaka.

Tayari Simba inawafikiria Wazambia wawili mmoja wao kuchukua nafasi ya Luis mmoja wao akiwa Justin Shonga. Miquissone amekuwa na mchango mkubwa katika kikosi cha Simba tangu alipojiunga nayo hasa msimu huu.

SOMA NA HII  USAJILI DIRISHA DOGO WAGAWA MASTAA SIMBA...AJIB, WAWA, MUGALU NA KIBU DENIS WATAJWA...