Home Habari za michezo BAADA YA KUANZA MAISHA MAPYA NA SIMBA….PHIRI KWA MARA YA KWANZA KAFUNGUKA...

BAADA YA KUANZA MAISHA MAPYA NA SIMBA….PHIRI KWA MARA YA KWANZA KAFUNGUKA HAYA YA MOYONI…


MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Simba, Mzambia Moses Phiri amepata dawa mpya ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Phiri ameweka wazi kwamba yuko fiti kucheza nafasi ngumu zaidi ya moja kikosini kulingana na matakwa ya Kocha Mserbia Zoran Maki.

Mchezaji huyo alisema msimu uliopita akiwa na Zanacco alikuwa akitumika kama mshambuliaji wa mwisho na kufunga mabao katika michezo mingi mfululizo ila kabla ya hapo alitumika kama winga nyuma ya mshambuliaji wa kati.

Raia huyo wa Zambia alisema akiwa Simba kwenye mechi mbili za kimashindano amecheza kama straika na amefunga mabao mawili na anaamini huo utakuwa mwendelezo wake.

“Jukumu la kwanza ambalo nilipewa na benchi la ufundi kuhakikisha nafunga mabao kama nafasi hiyo inavyohitaji. Binafsi nashukuru nimefanya kile ambacho kinachohitajika kwani ni silaha kwa timu kupata ushindi,” alisema Phiri na kuongeza;

“Ikitokea nikatumika kama winga upande wowote ule naamini ninao uwezo wa kufunga, kutengeneza nafasi za kufunga kwa wachezaji wengine pamoja na kushuka chini kusaidia kukaba kama majukumu ya nafasi hiyo yanavyohitaji mchezaji kufanya.

“Hata nikitumika nyuma ya mshambuliaji hapo napo hakuna shida yoyote nitakuwa kiunganishi kati ya viungo na straika ingawa nyakati nyingine kulingana na nafasi zilivyo nitajitahidi kufunga.

“Kuna wakati nilienda nje ya Afrika kwenye hiyo timu kocha alinipanga kama beki wa kulia nilimfanyia kazi nzuri mwenyewe hakuamini,” alisema Phiri na kusisitiza kwamba kama Zoran akimtaka asimame kwenye ulinzi yuko tayari muda wowote.

Mchezaji huyo alisema amebarikiwa kuwa hivyo na Mungu tangu akiwa mdogo amekuwa akicheza nafasi zote uwanjani kasoro kipa ambayo aliwahi kujaribu huko nyuma na ikamshinda.

“Naamini katika kila timu kuna ushindani inaweza kutokea unacheza nafasi moja tu halafu kuna mchezaji hapo ndio anatumika zaidi nikihamishwa kwenda eneo lingine siwezi kushindwa kucheza nitafanya vizuri pia huko,” alisema Phiri ambaye mechi na Yanga hakuchezeshwa na kuibua maswali kwa mashabiki.

Kocha wa Simba, Zoran Maki alisema Phiri akizoea mazingira ya Tanzania na ufiti wake ukiongezeka zaidi ya wakati huu anaweza kufanya vizuri katika kila mechi zaidi ya alivyofanya katika michezo miwili ya awali.

SOMA NA HII  GOMES AWAWASHIA TAA YA KIJANI NDEMLA NA GADIEL MICHAEL

“Nimefurahishwa na kujituma kwake hakuwepo katika mechi ya Yanga ila wakati tunafanya mazoezi ya Ligi Kuu Bara alikuwa katika kiwango bora na nikampa nafasi ya kuanza hakuniangusha amefunga katika michezo yote miwili,” alisema Zoran na kuongeza;

“Nataka kila mchezaji awe na moyo wa kupambana na kujituma kama hivi katika kila nafasi anayocheza kwani hiyo ndio moja wapo ya silaha ya kushinda michezo mingi.”