Home Habari za michezo BAADA YA KUONA WAMEZIDIWA KILA KITU …BEKI SIMBA AKUBALI YAISHE…AKUBALI YANGA BINGWA...

BAADA YA KUONA WAMEZIDIWA KILA KITU …BEKI SIMBA AKUBALI YAISHE…AKUBALI YANGA BINGWA MSIMU HUU..


PENGO la pointi lililopo baina ya Simba na Yanga katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, imemfanya beki wa zamani wa Wekundu wa Msimbazi, Salim Mbonde, kukiri chama lake msimu huu iusahau ubingwa, kwani wamezidiwa ujanja na watani.

Kabla ya mechi ya juzi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Yanga iliizidi Simba kwa jumla ya pointi 13, licha ya kuitangulia mechi za kucheza, Vijana wa Jangwani wamecheza mechi 20 na kukusanya pointi 54, ilihali Wekundu wa Msimbazi wamecheza michezo 19 na kuvuna pointi 41.

Jambo hilo limemfanya Mbonde aliyesajiliwa na Simba misimu minne iliyopita akitokea Mtibwa Sugar, alisema kwa sasa ni suala la muda tu Yanga kukabidhiwa taji la msimu huu huku akikiri timu hiyo imekuwa bora zaidi ya wapinzani wao.

“Ni msimu wa Yanga baada ya kusota miaka minne mfululizo wakiwaacha Simba wakifanya kile wanachostahili kutokana na ubora waliokuwa nao sasa wao wamechoka wameishiwa mbinu ndio maana wanajikuta wanaachwa nyuma sana,” alisema Mbonde na kuongeza.

“Simba imeshindwa kufanya mabadiliko ya kikosi chao ambacho kimetumika muda mrefu ndio kilicho waangusha wachezaji wengi wanaotumika sasa wamechoka walihitaji mapumziko.”

Alisema Simba haiko vibaya ina kikosi kizuri na cha ushindani shida iliyopo ni uchovu kwa wachezaji wamekuwa na mechi nyingi ligi na kimataifa na zote wameweza kufika hatua ileile waliyofika ndani ya misimu minne.

SOMA NA HII  KAMATA 'MAOKOTO' MARA MBILI YA DAU LAKO KUPITIA CASINO YA AGE OF THE GODS SPIN...