Home Habari za michezo WAKATI ISHU YA ONYANGO IKIWA BADO JUU JUU…MBRAZILI SIMBA AIBUKA NA MAELEKEZO...

WAKATI ISHU YA ONYANGO IKIWA BADO JUU JUU…MBRAZILI SIMBA AIBUKA NA MAELEKEZO HAYA..

Habari za Simba SC

Roberto Oliveira, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa ni wakati wa mabeki wa timu hiyo kuongeza umakini na kutimiza majukumu kwa wakati kwenye mechi watakazocheza.

Ipo wazi kwamba Simba imepishana na ubingwa wa ligi ambao upo mikononi mwa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Yanga pia imecheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika wakigotea kwenye nafasi ya mshindi wa pili huku mabingwa wakiwa ni USM Alger ya Algeria.

Timu hiyo inafanya maandalizi kwa mechi mbili za ligi zijazo ambapo ni dhidi ya Polisi Tanzania Juni 6 na Coastal Union Juni 9 zote zinatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.

Timu hiyo imeanza maandalizi kuelekea mechi hizo mbili ambazo zinatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu zote kupigia hesabu pointi tatu.

Raia huyo wa Brazil amesema kuwa kwenye kila idara katika kikosi hicho ni muhimu kuwa imara ili kupata matokeo mazuri.

“Kazi kubwa ipo kwenye kutafuta matokeo na ni muhimu kucheza kwa umakini kuanzia kwenye safu ya ulinzi na ushambuliaji hili ni muhimu kufanyika kwa wakati.

“Ukweli ni kwamba wachezaji wa Simba ni imara na wanafanya kazi kwa ushirikiano ikiwa ni kuanzia mabeki kuna Inonga, (Henock), Joash, (Onyango), Mohamed, (Hussein) kikubwa ni kuendelea kufanya kazi kupata ushindi kwenye mechi ambazo zimebaki,”.

Simba ikiwa imecheza mechi 28 na kukusanya pointi 67 imegotea nafasi ya pili huku ukuta ukiwa umefungwa jumla ya mabao 15 kibindoni.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONGEZA MKATABA YANGA JANA...FARID MUSA AMPA 'KIBARUA' OSCAR OSCAR WA EFM...