Home Yanga SC JEMBE JIPYA LAANZA MAZOEZI NDANI YA KIKOSI CHA YANGA

JEMBE JIPYA LAANZA MAZOEZI NDANI YA KIKOSI CHA YANGA


INGIZO jipya ndani ya kikosi cha Yanga, beki wa kati Dickoson Job ameanza mazoezi kwa ajili ya kuanza kazi kwenye maisha mapya ambayo yupo kwa sasa.

Job ni usajili wa Cedric Kaze ambaye alikuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Kaze alifutwa kazi Machi 7,2021 kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni matokeo mabovu ya timu hiyo.

Mpaka sasa Job hajacheza mechi yoyote ya ushindani baada ya kujiunga na Yanga akitokea Klabu ya Mtibwa Sugar kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya nyama za paja.

Kwa sasa tayari ameshapona na ameshaanza mazoezi pamoja na wachezaji wenzanke walio chini ya Kaimu Kocha, Juma Mwambusi.

Job amesema:”Ninamshukuru Mungu nipo salama na tayari kwa ajili ya kuwatumikia wana Jangwani.

“Furaha yangu kuwa ndani ya kikosi cha Yanga na matumaini yangu ni kuona kwamba ninafanya vizuri kila wakati,” .

Kwenye msimamo Yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 50 baada ya kucheza jumla ya mechi 23.

SOMA NA HII  KAZE AWATIMUA AKINA MUKOKO KAMBINI