Home Azam FC LWANDAMINA ASHTUKIA MCHONGO AZAM, AVUNJA MAPUMZIKO

LWANDAMINA ASHTUKIA MCHONGO AZAM, AVUNJA MAPUMZIKO


KOCHA mkuu wa klabu ya Azam, George Lwandamina ameshtukia mchongo, hii ni baada ya kuahirisha mapumziko ya wiki mbili ya kikosi chake, na kuamuru nyota wote ambao hawajaitwa kwenye vikosi vya timu ya taifa warudi kambini kujiandaa ma maandalizi ya michezo yao ijayo.

Hapo awali Azam walipanga kuwa na mapumziko ya wiki mbili ili kupisha ratiba ya michezo ya kimataifa, lakini wakaamua kubadili haraka mpango huo na kuwarudisha nyota wote ambao hawajaitwa kwenye timu za taifa ili kuanza mazoezi.

Azam inakamatia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi na pointi zao 44 walizokusanya baada ya kucheza michezo 24, huku wakizidiwa kwa pointi mbili tu dhidi ya Simba walio kwenye nafasi ya pili na pointi zao 46 baada ya kucheza michezo 20.

Akizungumzia uamuzi huo, Mkuu wa Kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Azam, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ alisema: “Tofauti na mpango wetu wa mwanzo wa kuipa timu mapumziko ya wiki mbili kupisha ratiba ya michuano ya kimataifa.

“Kuendana na mahitaji ya uongozi kwa kushirikiana na benchi la ufundi lililo chini ya kocha George Lwandamina tumefanya mabadiliko kidogo na tayari kikosi kimerejea kambini na kuanza mazoezi.

“Hii ni kwa sababu tunataka kuhakikisha wachezaji wetu wanakuwa na utimamu wa mwili wa kutosha ili kuweza kufanya vizuri katika michezo yetu ijayo, kwa kukusanya pointi nyingi zaidi kwenye michezo yetu ijayo ambazo bila shaka zinaweza kutupa nafasi ya kushindania ubingwa,”

SOMA NA HII  SIMBA SC KUMBE NI MAKAO MAKUU YA AZAM FC...AMRI KIEMBA AFICHUA SIRI HII