Home KMC FC KMC KUWA NA NYOTA WA KAZI ZAIDI YA 30 MSIMU UJAO

KMC KUWA NA NYOTA WA KAZI ZAIDI YA 30 MSIMU UJAO

UONGOZI wa Klabu ya KMC umeweka wazi kwamba kwa msimu ujao utakuwa na kikosi kazi ambacho kitajumuisha jumla ya wachezaji 30.
KMC yenye maskani yake Kinondoni ilimaliza ligi msimu uliopita wa 2020/2021 ikiwa nafasi ya tano kwenye msimamo baada ya kufikisha jumla ya pointi 48.
Kwa sasa sasa kikosi hicho bado hakijatangaza nyota ambaye wamemalizana naye huku nyota wake David Bryson akitangazwa kuwa mali ya Yanga.
 Katibu wa KMC, Walter Harrison amesema kuwa timu hiyo inatarajiwa kuingia kambini mwishoni mwa mwezi huu kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.
“Tunatarajiwa kuwa na wachezaji 30 ama 40 kwa kikosi kizima itategemea na mahitaji. Maandalizi yanakwenda vizuri na tumejipanga.
 
“Inshu ya usajili unaendelea katika hatua za awali na tutakapofanikisha tutawajuza mashabiki wa KMC kuhusu usajili wetu. Kuhusu kambi tunategemea kuingia mwezi huu,” amesema Harrison.
 

SOMA NA HII  KMC WAIPIGIA HESABU NAFASI YA NNE LIGI KUU BARA