Home Yanga SC YANGA YATOA TAMKO KUHUSU GSM

YANGA YATOA TAMKO KUHUSU GSM


 MSHINDO Msolla, Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga amesema kuwa wale ambao wanasema kwamba mdhamini wao Kampuni ya GSM hana msaada ndani ya timu hiyo huyo atakuwa sio mwenzao kwa kuwa haoni kile ambacho kinafanywa na mdhamini huyo.

Hivi karibuni baadhi ya mashabiki wamekuwa wakitajwa kulaumu uwepo wa wadhamini wa GSM wakidai kwamba hao wamekuwa watendaji badala ya uongozi jambo linalofanya timu kuyumba.

Msolla ameweka wazi kwamba ndani ya Yanga kila mmoja anatimiza wajibu wake kwa kufanya kile ambacho kinamhusu bila ya kuingiliana katika madaraka.

“Kila mmoja anafanya kazi yake, ikiwa kuna shabiki ambaye hataki GSM kuwa ndani ya Yanga huyo atakuwa sio mwenzetu kwa sababu hatambui yale ambayo wadhamini wetu wanafanya.

“Kwetu sisi sio wadhamini pekee bali wamekuwa ni patna katika kazi zetu na kila mmoja anatimiza majukumu yake kwa wakati.

“Mazingira ambayo tulianza nayo awali yanajulikana ila kupitia hawa GSM wameweza kulipa kambi ambayo timu imekuwa ikiweka, tulianza nao pale Legency alilipa miezi sita na kwa sasa tupo Avic ni mwaka mzima amelipa,” amesema.

Chini ya Injinia Hersi Said ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya GSM, Yanga imeweza kuhama kambi kutoka Legency na sasa ipo Kigamboni ambapo inaendelea na maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara.

SOMA NA HII  FT: YANGA 5-0 POLISI TZ.....GUEDE AFUTA GUNDU KIBABE....G5 ZA GAMONDI BADO WAARABU TU...