Home epl MANCHESTER UNITED WAPO TAYARI KUMSIKILIZA de GEA

MANCHESTER UNITED WAPO TAYARI KUMSIKILIZA de GEA


 IMERIPOTIWA kuwa Klabu ya Manchester United imeanza mazungumzo na kipa wake namba moja David de Gea ili kumsikiliza ofa yake.

Ripoti zinaeleza kwamba United itamsikiliza kipa huyo kile anachokihitaji na itampa ruksa ya kufanya chaguo analotaka yeye bila kumbana kwa  kuwa amefanya nao kazi kwa ukaribu na muda mrefu.

Ikiwa David de Gea akaamua kasepa ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Ole Gunnar Solskjaer itakuwa ni nafasi kwa Dean Henderson kuwa kipa namba moja.

Tayari Ole Gunnar Solskjaer ameanza kumuamini kijana Henderson kikosi cha kwanza lengo ikiwa ni kumjengea hali ya kujiamini ili aweze kurithi mikoba ya de Gea ambaye ameanza kikosi cha kwanza kwenye jumla ya mechi 434.



SOMA NA HII  PAMOJA NA KUIPELEKA RS BERKANE NUSU FAINAL SHIRIKISHO...IBENGE APATA AJALI MOROCCO...