Home Uncategorized BAADA YA SIKU 23, OKWI KUKINUKISHA SIMBA

BAADA YA SIKU 23, OKWI KUKINUKISHA SIMBA


HUKO ulipo weka kumbukumbu kabisa kwamba itakapofika Julai 19, straika wa Simba, Emmanuel Okwi ndiyo itakuwa siku ambayo ataanika juu ya mustakabali wake ndani ya kikosi hicho.

Okwi amemaliza mkataba wake ndani ya Simba ambapo kwa sasa straika huyo amekuwa akichengachenga kusaini mkataba mpya ndani ya kikosi hicho.

Mshambuliaji huyo ambaye kwa sasa yupo na timu ya taifa ya Uganda kwenye michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon), ameweka wazi kwamba itakapofika Julai 19, siku ambayo michuano hiyo inayofanyika nchini Misri kufikia tamati, ndipo atatoa msimamo wake wa kubakia ama kuondoka Simba.

Kuanzia leo hadi Julai 19, mwaka huu, zitakuwa zimepita siku 23 ambapo ndipo Okwi ataweka wazi mustakabali wake. “Hilo swali la mimi kubakia au kuondoka hapa Simba jibu lake litapatikana baada ya kumalizika kwa mashindano haya ya Afcon,” alisema Okwi.

Okwi anatarajiwa kuondoka Simba baada ya awali kuelezwa kuwa anataka kwenda Afrika Kusini au nchini Misri. Hata hivyo, Simba bado wanaonekana kuwa wanataka saini ya mshambuliaji huyo mahiri kwenye soka la Tanzania.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA YANGA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA AZAM FC