Home Habari za michezo YANGA HALI TETE LIGI YA MABINGWA ALLY KAMWE ATOA KAULI TATA

YANGA HALI TETE LIGI YA MABINGWA ALLY KAMWE ATOA KAULI TATA

Afisa Habari wa Yanga SC Ally Kamwe

Yanga SC wameingia unyonge baada ya kupangwa kundi D na klabu za Al Ahly,CR Belouzdad na Medeama ya Ghana katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Alichokiandika Afisa Habari wa Yanga Ally Kamwe kwamba wanaenda kupima kikosi cha mbele ya timu zenye ubora ni wazi kwamba wameshaona hawana uwezo wa kuvuka hatua hiyo.

Hata mashabiki wa Yanga nao wameingia unyonge ambapo kwao kufika hatua ya makundi ndio ilikuwa lengo la Klabu yao na hayo mengine ikitokea itakuwa ni bonasi tu.

Hatua ya Makundi ndio eneo ambalo Yanga wanapaswa kuonyesha ubora wao na kuweka standard yao Kimataifa kama vile Simba ambao hii hatua hawana wasiwasi nayo.

SOMA NA HII  HUYO MRITHI WA MAYELE HATARI ZAIDI YA MIL 400, MSHAHARA WAKE BADO MAJANGA