Home Habari za michezo FEI TOTO: HAWA SIMBA HAMNA KITU…TUMEWAZIDI KILA KONA…WASIJISUMBUE NA UBINGWA…

FEI TOTO: HAWA SIMBA HAMNA KITU…TUMEWAZIDI KILA KONA…WASIJISUMBUE NA UBINGWA…

Habari za Yanga

Baada ya Simba kuangusha pointi nyingine mbili dhidi ya Mbeya City, staa wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ametamka kwamba huu ni mwaka wao tena na kuna kila dalili kuwa hakuna wa kuwazuia kirahisi.

Kiburi cha Fei Toto kimeenda mbali zaidi na kudai kitakwimu mpaka sasa wao Yanga kama wakishinda mechi zao zote watakuwa wamewazidi watani wao, Simba kwa pointi 7 au zaidi kwani hawajajua mechi zinazofuata za Mnyama mkoani itakuwaje.

Yanga inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 29 sawa na Azam lakini kwa tofauti ya mabao huku Simba ikibaki nafasi ya tatu kwa pointi 28 na Singida ya nne pointi 21.

Kwenye takwimu za mechi za ugenini, Yanga imevuna pointi 18, ikifuatiwa na Geita 12, Azam 10 na Simba ya nne pointi tisa.

Fei Toto alitamba kwamba haoni kama kuna timu ambayo inaweza kuzuia kasi yao ya ushindi na kuwanyima taji la ubingwa kama Simba iliyoanza vizuri imeanza kuchemka.

Mchezaji huyo anasema kwamba timu nyingi hazichezi kitimu kama ambavyo wanacheza wao katika kutafuta ushindi uwanjani na ndio maana zinakwama kirahisi hata kwenye mechi zenye uzito wa kawaida.

“Timu nyingi zinategemea ubora wa mchezaji mmoja mmoja, ukiangalia timu yetu tunacheza kama timu moja hatuna ile kwamba timu ikimkosa huyu haipati matokeo, ndio maana kila mtu akiona amepata nafasi anataka kufanya kweli,” alisema Fei Toto huku akiongeza.

“Hili pekee linatupa ubora mkubwa wa kushinda mechi zetu,sioni anayeweza kutuzuia na tunalichukua tena hili Kombe watu wataona baadaye, ”alitamba mchezaji huyo na kuongeza pia kuwa ubora wa wachezaji wanaounda kikosi chao sambamba na benchi lao la ufundi uko juu hatua ambayo imeimarisha ushindani.

Alisema hakuna mchezaji ambaye kama atakaa nje atafurahia kuendelea kuwa nje kutokana na kuhofia kupoteza nafasi.

“Hapa Yanga siri kubwa ni ushindani wa nafasi pia, kikosi kina watu bora sana angalia alitoka kepteni (Bakari Mwamnyeto) akaingia Bacca lakini timu bado iko salama kwenye ile mechi iliyopita.”

“Hii sio kila timu inaweza kuwa na ubora wa ushindani kama huu kikosi chetu ni kipana sana ambacho kinajitofautisha na timu nyingine,” alisema Fei Toto mchezaji wa zamani wa JKU ya Zanzibar ambaye alianza kuichezea Taifa Stars 2018.

Ligi Kuu msimu huu imekuwa na ushindani mkali kutokana na uwekezaji uliowekwa na wadhamini.

SOMA NA HII  SABABU ZA MAYELE KUITIKISA YANGA ZAWEKWA WAZI MZIZE ATAJWA