Home Habari za michezo PHIRI MAMBO MAGUMU SIMBA, MKATA UMEME KUTOKA TOGO HUYU HAPA MSIMBAZI

PHIRI MAMBO MAGUMU SIMBA, MKATA UMEME KUTOKA TOGO HUYU HAPA MSIMBAZI

usajili simba

HUENDA muda wowote kuanzia leo, Simba inaweza kumalizana na straika wao raia wa Zambia, Moses Phiri ili kumpisha kiungo mkata umeme raia wa Togo, Novon Efoe.

Msimu uliopita, Efoe alikuwa akikipiga kwenye Klabu ya ASKO Kara ya kwao Togo, ambayo alijiungana nayo Novemba 1, 2020, akitokea AS Togo Port.

Chanzo chetu kutoka Simba, kimeliambia Spoti Xtra kuwa, uongozi wa Simba leo Jumapili unatarajia kukaa mezani na Phiri wamalizane ili wapate nafasi ya kumuingiza kiungo huyo.

“Jumapili kuna uwezekano mkubwa wa kumaliza mazungumzo na Phiri ili aweze kwenda kwa mkopo Zanaco United na nafasi yake tuitumie kuleta kiungo mpya, ambaye atasaidiana na Sadio Kanoute pamoja na Fabrice Ngoma.

“Tunaendelea kumshawishi Phiri akubali kuondoka maana hakutaka tangu mwanzo na kwamba anataka tumuache aende bure jambo ambalo hatujaafikiana, hivyo kama tutakubaliana kumtoa kwa mkopo basi kuanzia Jumatatu ijayo tutamtangaza kiungo mpya mkata umeme,” kilisema chanzo hicho.

Inaelezwa kwamba, Simba imekuwa ikitafuta kiungo mwingine mkabaji licha ya kumsajili Fabrice Ngoma, hiyo ni katika kuimarisha kikosi chao baada ya kuondoka kwa Jonas Mkude.

Katika nafasi hiyo ya kiungo mkabaji, ndani ya Simba hivi sasa inachezwa na Mzamiru Yassin, Sadio Kanoute na Fabrice Ngoma ambaye ni usajili mpya.

SOMA NA HII  GAMONDI,AUCHO WAFUNGUKA MAKALI YA YANGA