Home Yanga SC YANGA : TUNAMUUZA SARPONG KWA BILIONI 1.2

YANGA : TUNAMUUZA SARPONG KWA BILIONI 1.2


IMEFICHUKA rasmi kuwa klabu ya Yanga ipo tayari kumuachia mshambuliaji wao Michael Sarpong endapo tu kama kuna timu itakuwa tayari kulipa fedha kiasi cha shilingi bilioni 1.2 kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji huyo.

Sarpong mwenye uraia wa Ghana alijunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea katika klabu ya Rayon FC ya nchini Rwanda katika usajili wa dirisha kubwa, ambapo tangu ajiunge na timu hiyo amefanikiwa kuifungia mabao 4 katika michezo ya ligi kuu.

Chanzo chetu cha uhakika ndani ya Yanga kimetuambia kuwa kabla mshambuliaji huyo hajatua Yanga alitakiwa kujiunga na moja ya klabu kutoka china kwa kiasi cha shilingi bilioni 1.5, lakini dili hilo liliharibika kutokana na uwepo wa janga la Corona.

Hivyo kama wachina hao watamuhitaji tena Sarpong itabidi walipe bilioni 1.2 ili waweze kumpata maana kuna taarifa kuwa bado wachina hao wanamuhitaji Sarpong.

“Sarpong kabla ya kusajiliwa na Yanga alikuwa akihitajika ndani ya timu nyingi ndani na nje ya Afrika,kuna timu kutoka China ilikuwa tayari kumsajili kwa fedha ndefu zisizopungua Shilingi Bilioni 1.5, lakini dili lao lilikwama kutokana na uwepo wa janga la Corona ila kama kusingekuwepo na janga hilo basi Sarpong angekuwa anakipiga katika moja ya klabu inayoshiriki ligi ya china. 

“Wachina bado hawajakata tamaa ya kumuhitaji Sarpong kwani bado wanamfuatilia kwa ajili ya kujaribu kumsajili tena, Yanga wanaweza kumuachia Sarpong lakini itawalazimu kumnunua mshambuliaji huyo kwa shilingi Bilioni 1.2 na kama hawatafikia hapo basi hawatampata,” Kilisema Chanzo hiko.

SOMA NA HII  KWA HIKI KITASA KIPYA CHA YANGA...MASTRAIKA LIGI KUU WATAFUTE PA KUPITA....JAMAA NI RAMOS MTUPU......