Home Habari za michezo YANGA YAGEUKA TISHIO AFRIKA…… ISHU IKO HIVI

YANGA YAGEUKA TISHIO AFRIKA…… ISHU IKO HIVI

Habari za Yanga leo

Kocha huyo anayokumbukumbu ya kupokea kichapo cha mabao 2-0 wakiwa nyumbani katika mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Al Merrikh wanatarajiwa kurudiana na Yanga katika mchezo wa mzunguko wa pili wakiwa ugenini katika Uwanja wa Azam Comlex mchezo huo unatarajiwa kufanyika Septemba 30.

Akizungumza kuelekea katika mchezo wa marudiano dhidi ya Yanga kocha huyo alisema kuwa: “Ukisema kuwa tunahofia kukutana na Yanga hapana, hilo halina ukweli kwa kuwa tayari tulishacheza nao na tulipoteza mchezo wa kwanza, ukweli ni huu kuwa Yanga kwa sasa ni tishio Afrika kulingana na walivyo.

“Ni timu ambayo inacheza vyema na inapata matokeo hivyo ni lazima tuwaheshimu kulingana na ubora wao huo, tunakwenda kurudiana na timu ambayo ni ngumu lakini wakiwa na faida kubwa ya wao kucheza kwao.

“Ambacho kipo kwa upande wetu ni kuendelea kujipanga kwa ajili ya kuhakikisha kuwa tunafanya vyema, kuwa na mipango mizuri ya kupata matokeo tukiwa ugenini, nia na malengo yetu ni kwenda hatua inayofuata na tuna matumaini hayo na wala hatujakata tama,” alisema kocha huyo.

SOMA NA HII  KUMBE KIPIGO CHA YANGA JANA KINAHISTORIA KUBWA AISEE...HUWA NI KAWIADA YAO 'KUBONDWA'...