Home Habari za michezo KUMBE KIPIGO CHA YANGA JANA KINAHISTORIA KUBWA AISEE…HUWA NI KAWIADA YAO ‘KUBONDWA’…

KUMBE KIPIGO CHA YANGA JANA KINAHISTORIA KUBWA AISEE…HUWA NI KAWIADA YAO ‘KUBONDWA’…

Yanga Tunisia

Matokeo ya Yanga kupoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Monastir ya Tunisia huko Tunis leo, yameendeleza mkosi wa wawakilishi hao wa Tanzania katika mechi za kwanza za hatua ya makundi ya mashindano Afrika.

Yanga haijawahi kupata ushindi katika mechi ya kwanza mara zote ambazo imewahi kuingia hatua ya makundi ya mashindano ya klabu Afrika ambazo ni mwaka 1998, 2016, 2018 na msimu huu.

Katika awamu hizo nne tofauti ambazo Yanga ilifanikiwa kutinga hatua ya makundi, kwenye mechi ya kwanza ilitoka sare mara moja na kupoteza mara tatu.

Yanga ilianza kucheza hatua ya makundi ya mashindano ya klabu Afrika kwa mara ya kwanza mwaka 1998 kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo mechi ya kwanza walitoka sare ya bao 1-1 na Manning Rangers ya Afrika Kusini.

Mara ya pili kwa Yanga kucheza hatua ya makundi ya mashindano ya Klabu Afrika ilikuwa ni 2016 walipofanya hivyo kwenye Kombe la Shirikisho Afrika ambapo mchezo wa kwanza wa hatua hiyo walianza kwa kufungwa bao 1-0 na MO Bejaia ya Libya.

Kwa mara nyingine tena, mechi ya kwanza ya hatua ya makundi iliendelea kuitesa Yanga mwaka 2018 walipopoteza kwa mabao 4-0 mbele ya USM Alger katika Kombe la Shirikisho Afrika.

SOMA NA HII  LUIZ KUIBUKIA SERIE A