Home Uncategorized JINA LA YONDANI LAUNGANISHWA NA NGASSA KUIBUKIA GWAMBINA

JINA LA YONDANI LAUNGANISHWA NA NGASSA KUIBUKIA GWAMBINA

 

KELVIN Yondani, mkongwe aliyezipiga Simba na Yanga kwa nyakati tofauti jina lake inaelezwa kuwa limeunganishwa na la Mrisho Ngassa kuibukia ndani ya Gwambina FC ya Mwanza.


Wachezaji hawa wote wawili walikuwa wanakipiga Yanga pamoja kwa msimu wa 2019/20 kabla ya panga kuwapita ambapo kwa sasa ni wachezaji huru.

Ngassa mkataba wake uliisha ndani ya Yanga uongozi uliachana naye jumla, kisha Yondani ambaye naye mkataba wake uliisha walikuwa kwenye mazungumzo ya kuongeza mkataba waliposhindwana naye akapewa mkono wa kwa kheri.

Habari zinaeleza kuwa Gwambia ambayo msimu wa 2020/21 itashiriki Ligi Kuu Bara baada ya kupanda kutoka Ligi Daraja la Kwanza imeanza kujiimarisha ili kuleta ushindani.

Habari kutoka ndani ya Gwambina FC zimeeleza kuwa tayari mchakato wa usajili umeanza huku majina ya wakongwe yakitajwa kusajiliwa.


“Kuna wakongwe ambao wanatazamwa ili kusajiliwa ndani ya Gwambina ikiwa ni pamoja na wale ambao wapo huru kama Yondani na Ngassa, hawa wanaweza kuongeza makali ndani ya kikosi,” ilieleza taarifa hiyo,


Katibu Mkuu wa Gwambina FC, Daniel Kirahi amesema kuwa wamepanga kusajili wachezaji nane pekee huku akigoma kuzungumzia ishu ya Yondani na Ngassa.

SOMA NA HII  SIMBA HII MHH,YANGA WANAJAMBO LAO,KESHO NDANI YA SPOTI XTRA JUMAPILI