Home Uncategorized LEWANDOWSKI AYEYUSHA MATUMAINI YA CHELSEA KUTINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA

LEWANDOWSKI AYEYUSHA MATUMAINI YA CHELSEA KUTINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA

 

ROBERT Lewandowski nyota wa Bayern Munich alikuwa na jambo lake usiku wa kuamkia leo Kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Chelsea hatua ya 16 bora kwa kuwatungua mabao mawili yaliyowatua Chelsea kwenye reli.

Wakati wakishinda kwa mabao 4-1 mchezo uliochezwa Allianz Arena, Chelsea hawakuwa na chaguo zaidi ya kukubali yaishe.

Mabao yake Lewandowski alitupia dakika ya 10 kwa penalti na dakika ya 83 huku yale mengine yalifungwa na Ivan Perisic dakika ya 24 na Corentino Tolisso dakika ya 76.

Bao la Chelsea lilifungwa na Tammy Abraham dakika ya 44 ila halikuwasaidia Chelsea kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

SOMA NA HII  JEMBE LINALOPIGIWA HESABU NA SIMBA LAINGIA ANGA ZA YANGA