Home Habari za michezo WAKATI SIMBA NA YANGA ZIKIJIMWAYA MWAYA …WAZO LA UJENZI WA UWANJA WA...

WAKATI SIMBA NA YANGA ZIKIJIMWAYA MWAYA …WAZO LA UJENZI WA UWANJA WA MKAPA LILITOKA HAPA…

Habari za Michezo

Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya tatu, Frederick Sumaye amesema wazo la kujenga uwanja wa Taifa (zamani) na sasa Uwanja wa Mkapa lilitokana na yeye pamoja na aliyekuwa rais wake, Hayati Benjamin Mkapa.

Mzee Sumaye amesema hayo wakati akifanya mazungumzo maalum na kipindi cha Power BreakFast cha Clouds FM.

“Suala la ujenzi wa uwanja [Benjamin Mkapa Stadium] tulilijadili sana mimi na Mzee Mkapa, akanituma kwenda China kuongeanao ili watusaidie kujenga huo uwanja.”

“Nilifika China tukaongea na Waziri Mkuu wao, badae Waziri wao wa mambo ya Michezo akaja huku [Tanzania] tukajadili sana.”

“Kwa hiyo ni wazo ambalo Mzee Mkapa alikuwanalo na tukasaidiana kuhakikisha uwanja unajengwa. Aliniambia nisimamie hilo jambo kwa kushirikiana na Mawaziri waliokuwepo wakati ule.”

“Tunashukuru kwamba tulifanikiwa, ukweli ni kwamba nchi kubwa kama Tanzania ilikuwa haina uwanja wenye hadhi ya kimataifa. Unategemeaje maendeleo ya mchezo wa mpira wa miguu wakati hata uwanja wa kimataifa hauna.”

“Tuliona mapenzi ya watanzania kwenye mchezo wa mpira wa miguu tukaamua kujenga uwanja mkubwa wenye hadhi. Mzee Mkapa aliniambia anataka uwanja ukamilike kabla hajatoka madarakani.”

SOMA NA HII  RASMI....NABI AFUNGA FAILI LA FEI TOTO YANGA...ATUMA UJUMBE HUU KWA MABOSI JANGWANI...