Home Habari za michezo WAKATI YANGA ‘WAKIINUA KWAPA’ LA UBINGWA TZ…MAMBO YAKO ‘KOONI’ KWA NABI HUKO…

WAKATI YANGA ‘WAKIINUA KWAPA’ LA UBINGWA TZ…MAMBO YAKO ‘KOONI’ KWA NABI HUKO…

Habari za Michezo leo

Ligi Kuu ya Morocco maarufu kama Botola Pro imeendelea kuwa na ushindani mkubwa baada ya Raja Athletic Club kushinda Kiporo Chao juzi na kupunguza gepu la pointi mbele ya kinara Association Sportive des Forces Armées royales maarufu kama FAR Rabat au waweza waita ASFAR.

Raja Casablanca wameipa kisago kizito RS Berkane Cha mabao 3-0 na kuwafanya wafikishe alama 63 wakati FAR Rabat akiwa na alama 64 katika nafasi ya kwanza.

Bingwa atapatikana mechi mbili zijazo ili Nasreddine Nabi atwae Ubingwa lazima ashinde mechi zake zote zilizopo mbele yake ikiwemo ile ya Casablanca dabi dhidi ya Wydad Athletic Club.

Msimamo wa Ligi:
AS Far Rabat – alama 64
Raja Casablanca – alama 63
RS Berkane – alama 46
Wydad – alama 41

Njia ya Wydad Casablanca kutinga CAF Confederation Cup msimu ujao ni kuomba Raja Athletic Club na FAR Rabat wabebe Kombe la Mfalme msimu huu ambalo lipo hatua ya Nusu fainali hivi sasa.

SOMA NA HII  WAKATI YANGA WAKITAMBA KUWA NA BIGIRIMANA WAO....PACHA WAKE AIBUKIA KMC ...KUANZA MAJAMBOZI NA IHEFU...