Home Simba SC SIMBA QUEENS WADHAMIRIA KUFANYA MAAJABU KLABU BINGWA AFRIKA

SIMBA QUEENS WADHAMIRIA KUFANYA MAAJABU KLABU BINGWA AFRIKA


MABINGWA wa Ligi Kuu ya Wanawake nchini (WPL) Simba Queens wanatarajia kuingia kambini Juni 16 kujiandaa na michuano ya kimataifa.

Simba itaiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kanda inayotarajiwa kufanyika Kenya kuanzia Julai 17 mwaka huu baada ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo ikiwa imefikisha pointi 54 na kuwazidi watani zao Yanga Princess pointi 53.

Michuano hiyo itashirikisha timu kutoka nchi za Rwanda, Uganda, Ethiopia, Somalia, Djbout, Kenya na Sudan Kusini.

Akizungumza ushiriki wao katika michuano hiyo mpya ya Kimataifa kwa wanawake, Kocha Mkuu wa Simba Queens Mussa Mgosi alisema, wanatarajia kujiandaa zaidi ili kufanya vizuri.

Alisema, anajua na kutambua ushindani utakuwa mkubwa hivyo ni wajibu wake kama kocha kuitengeneza timu iweze kushindana na sio kushiriki.

“Nawaheshimu sana wapinzani wetu wote ambao tutakutana nao katika michuano hiyo, bila kujiandaa ni kazi bure, kwasasa wachezaji wako majumbani mapumziko mafupi, Juni 16 wanarudi kuendelea na majukumu,”alisema Mgosi.

Alisema, atahakikisha anapambana ili nyota wake wafanye vizuri katika michuano hiyo ambayo bingwa ndiye atawakilisha ukanda katika michuano ya Afrika itakayofanyika nchini Morroco baadaye mwaka huu.

SOMA NA HII  SIMBA KAMILI GADO KWA AJILI YA WASUDAN