Home Simba SC SIMBA KAMILI GADO KWA AJILI YA WASUDAN

SIMBA KAMILI GADO KWA AJILI YA WASUDAN


 DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Al Merrikh ya Sudan.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Machi 6 utakuwa ni wa tatu kwa Simba ndani ya kundi A ambapo inaongoza ikiwa na pointi sita.

Kikosi kinatarajiwa kuanza safari leo kuibukia nchini Sudan ili kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo huo huku habari zikieleza kuwa tayari mabingwa hao watetezi wameshawatuma watu wao mapema nchini Sudan.

“Tayari wapo waliotangulia nchini Sudan kwa ajili ya kuweka mazingira sawa. Ipo wazi kwamba maandalizi ya mpira huwa yanaanza mapema hilo ndilo ambalo linafanyika pia ndani ya Simba,” .

Baada ya kumaliza mchezo wao wa jana kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Tanzania, Gomes amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo.

Kocha huyo ambaye ameongoza kikosi hicho kwenye jumla ya mechi tisa akiwa na kombe moja kabatini la Simba Super Cup ameweza kuanza vizuri ndani ya kikosi hicho baada ya kuchukua mikoba ya Sven Vandenbroeck.

SOMA NA HII  GOMES AFUNGUKA SABABU ZA MKUDE KUKOSEKANA SIMBA