Home Habari za michezo FEI TOTO AVUNJA UKIMYA …AANIKA ISHU YAKE NA SIMBA…AMTAKA INJINIA HERSI AONDOKE...

FEI TOTO AVUNJA UKIMYA …AANIKA ISHU YAKE NA SIMBA…AMTAKA INJINIA HERSI AONDOKE YANGA..

Tetesi za Usajili Yanga

Baada ya kupiga kimya kwa muda mrefu tangu kuibuka kwa sakata lake la kutaka kuvunja Mkataba na Klabu yake ya Yanga, Kiungo wa Yanga Feisal Salum hatimaye ameamua kufunguka kwa nini anataka kuvunja Mkataba na Klabu ya Yanga.

Wakati waliokuwa wengi wakishauri kuwa alipaswa kusubiri Mkataba wake uishe ndipo adai maslahi mapana, kiungo huyo ameweka wazi kuwa alikataa kujiunga Simba SC kwa dau kubwa akachagua kucheza Yanga.

Akizungumza Feisal kupitia Redio ya Clouds FM Feisal anasema;

“Nafsi yangu ilitamani kwenda kuchezea Yanga, nilikubali kwenda kuichezea Yanga kwa kipato kidogo zaidi ya kile ambacho nilikikataa Simba SC, ni kwasababu ya mapenzi tu”

Aidha amesema kuwa Kitendo cha kukaa pasipo kucheza mpira hata yeye hakipendi kwa kuwa yeye ni mtoto wa Kimasikini na ili apate kipato lazima acheze mpira.

Mbali na hilo Mchezaji huyo amedai mzazi wake ni mgonjwa na yeye ndio anasimamia matibabu hivyo pasipo kupata pesa kupitia kucheza mpira kwake inakua shida.

“Mimi nimetokea kwenye familia ya kimasikini, mimi nasaidia familia yangu, ili mambo yaende ni lazima mimi nifanye kazi, Baba yangu anaumwa na mimi ndio nasimamia matibabu, yeye mwenyewe hapendi hili sakata liendelee kwasababu kuna mambo yanakwama”

Katika hatua nyingine Fei amefichua kuwa m gogoro wake mkubwa ni dhidi ya Rais wa Yanga Injinia Hersi ambae ndio mkuu wa shughuli zote za Yanga hivyo kwa kuwa bado yupo ni ngumu yeye kurudi.

Fei ameenda mbali na kusema kuwa iwapo Rais wa Yanga Injinia Hersi atang’atuka hata sasa hivi basi yeye yuko tayari kurudi Yanga muda wowote kwa kuwa huyo ndio mtu mwenye mgogoro nae.

SOMA NA HII  UKWELI MTUPU....RATIBA LIGI KUU YAISHIKA PABAYA SIMBA...WAKIJITINGISHA TU..YANGA BINGWA TENA...