Home Uncategorized MTAMBO WA MABAO NAMUNGO WAGOMEA MKATABA MPYA WATAKA NAMBA YANGA

MTAMBO WA MABAO NAMUNGO WAGOMEA MKATABA MPYA WATAKA NAMBA YANGA

 INAELEZWA kuwa mshambuliaji wa Namungo FC, raia wa Burundi, Bigirimana Blaise, amekataa kuongeza mkataba wa kukipiga ndani ya klabu hiyo ili kutimiza ndoto zake za kujiunga na Yanga.

 

Taarifa za kuaminika kutoka kwa mtu wa karibu na Blaise zilisema, nyota huyo aliyemaliza ligi akiwa na mabao 10, amekuwa akimshinikiza meneja wake kufanya mpango wa kumtafutia nafasi ya kusajiliwa na Yanga, kwa kuwa ndoto zake kubwa ni kuona msimu ujao anavaa jezi ya timu hiyo.

 

 Habari za kuaminika kutoka ndani ya Namungo, zimeeleza: “Bigirimana amegoma kuongeza mkataba wa kubaki hapa Namungo kwa sababu tamaa yake kubwa ni kwenda kuichezea Yanga, amekuwa akisisitiza muda mrefu kuwa anatamani kuwa mchezaji wa timu kubwa kwa msimu ujao.”

 

 Bigirimana juu ya ishu hiyo amesema: “Kiukweli nataka kupata changamoto mpya msimu ujao, nimegoma kuongeza mkataba Namungo kwa sababu nataka kucheza timu nyingine. Masuala ya Yanga siwezi kusema, kama kweli yapo basi meneja wangu atakuja kuweka wazi.”

SOMA NA HII  MTAZAMO WA SALEH JEMBE KUHUSU SIMBA NA YANGA