Home Habari za michezo KUELEKEA MSIMU UJAO….KIFAA HIKI NACHO MBIONI KUTUA SIMBA…’NI STRAIKA NA NUSU’…HISTORIA YAKE...

KUELEKEA MSIMU UJAO….KIFAA HIKI NACHO MBIONI KUTUA SIMBA…’NI STRAIKA NA NUSU’…HISTORIA YAKE BABU KUBWA…


Imefahamika kwamba Simba ipo katika mipango ya kumsajili mshambuliaji wa Vipers SC ya Uganda, Yunus Sentamu, ambaye raia wa Uganda.

Simba imepanga kukifanyia uboreshaji kikosi chake katika baadhi ya nafasi kati ya hizo ni safu ya ushambuliaji ambayo imeonekana kutokuwa na ubora mzuri.

Wakimpata straika huyu inaelezwa kuwa tatizo hilo litakuwa limekwisha rasmi.

Sentamu msimu uliopita aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya Vipers kufunga mabao 16 ndani ya msimu mmoja na akawa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Uganda msimu huo wa 2020/21.

Safu ya ushambuliaji ya Simba inahitaji uboreshaji. Hivi sasa inaongozwa na Mnyarwanda Meddie Kagere, Mkongomani Chris Mugalu na nahodha John Bocco ambao katika baadhi ya mechi muhimu msimu huu walishindwa kuibeba timu.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo tumezipata, Sentamu anakuja kuchukua nafasi ya Mugalu ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa timu hiyo imetoa tenda kwa baadhi ya mawakala wakubwa kutoka nchini kwa ajili ya kuwatafutia wachezaji nafasi ya beki wa kati na washambuliaji, na kati ya hao yupo Sentamu.

Aliongeza kuwa uongozi wa timu hiyo, utampa mkataba straika huyo kama Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mhispania, Franco Pablo atampitisha katika usajili wake kama akivutiwa na kiwango chake baada ya kuziona baadhi ya video zake.

“Wapo wachezaji wengi wanaotajwa kuja kuichezea Simba katika msimu ujao, na nafasi ya kwanza ambayo ameuomba uongozi iifanyie maboresho ni safu ya ushambuliaji.

“Kocha Pablo anaamini kuwa safu hiyo ya ushambuliaji ndiyo imesababisha wao waondolewe katika hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

“Washambuliaji wake walionekana kukosa umakini kushindwa kutumia nafasi nyingi ambazo walikuwa wakizipata katika michezo yao ya Shirikisho msimu huu,” alisema mtoa taarifa huyo.

Pablo alithibitisha hilo hivi karibuni kwa kusema: “Ni lazima tukifanyie uboreshaji kikosi chetu katika baadhi ya maeneo na kati ya hayo mabeki wa kati na washambuliaji.

SOMA NA HII  YANGA WAKUBALI YAISHE...WACHOMOA MPANGO WA KUPIGA KAMBI ULAYA...NABI ATAKA KAMBI IWE HAPA HAPA DAR...

“Kwani kama tungekuwa na safu nzuri ya ulinzi na washambuliaji, basi tungefika nusu fainali ya Shirikisho katika msimu huu, hivyo tutafanya usajili mzuri katika kuelekea msimu ujao.”

Sentamu ana umri wa miaka 27 na anaichezea timu timu ya taifa ya Uganda.