Home yanga GAMONDI AWAPIGA MKWARA HUU MASHUJAA…AMEFUNGUKA HAYA A-Z

GAMONDI AWAPIGA MKWARA HUU MASHUJAA…AMEFUNGUKA HAYA A-Z

Habari za Yanga leo

Kocha Mkuu wa Yanga, Angel Miguel Gamond amesema wanazitaka alama tatu kutoka kwa Mashujaa FC ili kuendelea kujihakikishia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu huu.

Yanga ambao wanahitaji alama 9 pekee kuwa mabingwa wa Ligi Kuu kwa mata ya 30, watashuka Dimbani leo katika Uwanja wa Lake Tanganyika kukipiga na Mashujaa FC ya Kigoma.

“Kwanza kabisa napenda kusema asante sana kwa Mashabiki wetu hapa Kigoma, mapokezi tuliyopata leo (jana) kutoka Uwanja wa Ndege mpaka hotelini sijaamini! hii inaonyesha ukubwa na upendo wa Mashabiki kwa Young Africans SC.

“Tumejiandaa vizuri na mchezo wa kesho (kesho) na tunafahamu utakuwa mchezo mgumu, sisi tunahitaji alama 3 na najua na Mashujaa na wao wana uhitaji mkubwa na alama hizi. Lakini ili tuwe mabingwa ni muhimu kupata alama 3 kwenye kila mchezo tunaocheza,” Miguel Gamondi.

SOMA NA HII  MITIHANI HII MIPYA YAMUUMIZA KICHWA FEI TOTO...BOCCO NA KIPRE WATAJWA