Home Habari za michezo ACHANA NA STORI ZA VIJIWENI…HUU HAPA UKWELI WA KWANINI KAMBOLE HATACHEZA MECHI...

ACHANA NA STORI ZA VIJIWENI…HUU HAPA UKWELI WA KWANINI KAMBOLE HATACHEZA MECHI YA LEO DHIDI YA SIMBA…


Kocha Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi amefunguka kuwa kwenye mchezo wa leo dhidi ya Simba watamkosa straika wao mpya, Lazarious Kambole.

Akizungumzia maandalizi yao katika mkutano na Wanahabari siku ya jana, Nabi amesema “Tunashukuru tupo sawa kuelekea kwenye mchezo wetu wa kesho dhidi ya Simba.

“Tumekuwa na maandalizi kwa muda mfupi lakini tumejitahidi kuendana na muda ila kikubwa tumejiandaa vizuri na tunatambua umuhimu wa mchezo huu kwamba unaangaliwa na nchi nyingi Afrika hivyo tuna imani tunaenda kupata matokeo.

“Tutamkosa Kambole kwenye mchezo huo kutokana na kusumbuliwa na majeraha lakini kwa upande wa Jesus Moloko yeye tayari ameanza mazoezi na timu hivyo atakuwa sehemu ya kikosi.

“Kwenye mchezo dhidi ya Vipers tulikuwa hatujajiandaa vizuri kutokana na muda ambao tuliingia kambini tofauti na Vipers lakini nilipata picha halisi ya kikosi changu na haikuwa lazima tupate matokeo katika ule mchezo.”

SOMA NA HII  FURAHIA UNAPOCHEZA KASINO YA MTANDAONI KWA SLOTI HII NDANI YA MERIDIANBET...