Home Habari za michezo #NGAOYAJAMII2022:..HAWA HAPA MASTAA WATAKAO AMAU MATOKEO YA DABI…WAKIZINGUA KILA JAMBO LIMEVURUGIKA…

#NGAOYAJAMII2022:..HAWA HAPA MASTAA WATAKAO AMAU MATOKEO YA DABI…WAKIZINGUA KILA JAMBO LIMEVURUGIKA…


Leo pale Uwanja wa Benjamin Mkapa kuna dakika 120 za heshima ambazo lazima kati ya watani Mabingwa wa Ligi Kuu Bara Yanga au wenzao Simba mmoja afungue msimu salama au kwa huzuni.

Ni katika mechi ya Ngao ya Jamii ambayo ni maalum kwa ajili ya kufungua pazia la Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23.

Msimu uliopita safari ya Yanga kuchukua mataji matatu ilianzia hapa wakiifunga Simba kwa bao 1-0 na hawa ni mastaa ambao wanaweza kuamua mchezo huu kutokana na ubora wao.

AZIZ KI NA HABIB KYOMBO

Yanga wana ingizo jipya msimu huu mshambuliaji Stephane Aziz KI ambaye anacheza pambano lake la kwanza la watani. Staa huyu sio mgeni wa nyavu za wekundu hao, amewahi kuwafunga mara mbili katika mechi mbili za nyumbani na ugenini alipokuwa akiitumikia ASEC Mimosas. Kama mabeki wa Simba wakijisahau wataumia.

Simba pia wana ingizo jipya katika safu yao ya ushambuliaji, Habib Kyombo. Fundi huyu mzawa sio mgeni katika nyavu za Yanga. Amewahi kuwatungua alipokuwa Mbao FC. Hazungumzwi kama mtu staa lakini anaweza kushtua kama mabeki wa Yanga nao watamdharau badala ya kumchunga.

KIBU NA MAYELE

Simba wanaye huyu mshambuliaji mwenye nguvu na kasi, Kibu Denis, ambaye msimu uliopita alikuwa mfungaji bora kwao akiwa katika mwaka wake wa kwanza tu Msimbazi. Huyu si mshambuliaji wa kuachwa kwani tayari ameanza kukamata kasi ya kucheka na nyavu.

Kule Yanga nako kuna mtu mwingine hatari, Fiston Mayele ambaye aliwafunga Simba katika mchezo kama huo msimu uliopita bao ambalo liliamua bingwa wa ngao kama hii.

Mayele ni hatari ingawa amekuwa akikutana na wakati mgumu kufunga tena mbele ya beki kisiki Henock Inonga wa Simba, lakini kama mabeki watamuachia nafasi ndogo usishangae kuona β€˜anatetema’.

FEISAL NA OKRAH

Yanga wana kiungo mwingine ambaye anaanza kuzizoea nyavu za Simba, Feisal Salum. Msimu uliopita katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) pale CCM Kirumba bao lake ndilo lililoamua mchezo na kama Simba hawatajua jinsi ya kumdhibiti anaweza kuwakumbusha kilio tena.

SOMA NA HII  PAMOJA NA LIGI KUWA BADO SANA....HIVI NDIVYO YANGA 'WALIVYOIKALIA SIMBA KIMTINDO'

Wakati Yanga wakiwa na Feisal, Simba wanaye fundi kabisa wa mpira, Augustine Okrah. Huyu ni mchezaji wa kiwango cha juu kabisa ambaye ameitwa hadi katika timu ya taifa ya Ghana iliyojaa wakali wanaocheza soka la kulipwa Ulaya. Yanga wanatakiwa kuwa naye makini kutokana na ufundi wake hasa mpira unapokaa katika mguu wake kushoto, kama atasahaulika unaweza kuwa usiku mchungu kwa Wanajangwani.

FARID NA OKWA

Winga Farid Mussa sio mtu ambaye anatakiwa kudharauliwa, ikumbukwe kasi yake na pasi yake jinsi ilivyozalisha bao pekee katika mchezo kama huu msimu uliopita bao likifungwa na Mayele.

Lakini Simba inaye fundi mwingine mpya Nelson Okwa kutoka Nigeria, ambaye wiki hii ameshtua alipowafungia Wekundu bao la pili katika mchezo wa Simba Day waliposhinda 2-0 dhidi ya mabingwa wa Ethiopia, St. George na amewahi kuwasumbua Yanga alipokuwa na Rivers United ya Nigeria. Akisahaulika atawaliza.

CHAMA NA SURE BOY

Fundi wa mpira Clatous Chama amerudi katika ubora wake na wiki hii amewakalisha watu chini sasa anawafuata Yanga ambao wanamjua kwamba jamaa akiwa katika ubora wake ni staa ambaye anatakiwa kuchungwa sana kwa pasi zake na hata kufunga.

Wakati Simba wakiwa na Chama, Yanga nao wana Abubakar Salum β€˜Sure Boy ambaye kama atapata nafasi anajulikana alivyohatari kutokana na pasi zake na hata kufunga kama atapata nafasi.

MORRISON NA SAKHO MORRISON NA SAKHO

Yanga wana mtu mwi-ngine hatari Bernard Morrison ambaye anaweza kuanzia benchini lakini kama ataingia anajulikana kwania amewahi kupeleka maumivu kwao kwa bao la ufundi mkubwa, hivyo sio mtu ambaye anatakiwa kuachwa kirahisi akafanya vitu kwa ubora wake.

Ila Simba wanaye mfungaji wa bao bora Afrika, Pape Sakho. Hajawahi kuifunga Yanga lakini kama akisahaulika atawapasua maana jamaa ana kasi, chenga na analijua goli.